Jimbo Katoliki Ifakara kwa mara ya kwanza limekutana na kufanya Ibada ya Hija ya Kijimbo na Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Kutukuka kwa Msalaba katika Parokia ya Bikira Maria Bibi yetu wa Kiberege
Published date, 2023-09-14Jimbo Katoliki Ifakara kwa mara ya kwanza limekutana na kufanya Ibada ya Hija ya Kijimbo na Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Kutukuka kwa Msalaba katika Parokia ya Bikira Maria Bibi yetu wa Kiberege ikitanguliwa na Mkesha kwa Sala na Mafundisho mbali mbali kuhusu Maana halisi ya hija na Msalaba. Misa ilitanguliwa na maandamano yaliyoratibiwa na dekani zote za Jimbo.Ibada imeongozwa na Mhashamu Baba Askofu Salutaris Libena Askofu Jimbo katoliki Ifakara. Kwa mara ya Kwanza Hija katika Dekania ya Kilombero ilianza mwaka 2014, ikiwa bado Kanisa halijajengwa, hata hivyo mipango iliyowekwa na Halmashauri kuu ya walei chini ya Baba Hospitio Itatilo
ambae ni Makamu wa Askofu, pamoja na Pd.Rwegoshora imefanikisha kuweza kuwa na wazo la Kukutanisha Dekania Zote za Jimbo kuendelea kukutana kwa Hija. Hija ni safari, imeanza mwaka wa Kwanza wa ukristo ambapo waamini wale wa Kwanza walikuwa na hamu ya kutembelea Sehemu zile Takatifu wakiwa na lengo la kwenda kusali huko ili kujichotea baraka, hata hivyo huduma hiyo ilitanuka kw kuhamia katika ngazi za mitume katika makaburi ya watakatifu kule Roma. Kanisa pia lilipitisha Sehemu aliyozaliwa Mama Bikira Malia kama Sehemu ya Hija. Hata hivyo Majimbo pia yamepewa kibari kuwa na Sehemu za Hija. Yafuatayo ni maeneo ya Hija kwa Jimbo katoliki I
fakara: Dekania ya Mlimba ni:- Kanisa la Ekaristi Takatifu Mpanga. Dekania ya Mchombe na Mofu ya sasa, kutoka Kanisa la Mt.Yohane Mtume Mchombe Dekania ya Ifakara: Kanisa kuu la Jimbo Dekania ya Kilombero:Kiberege na ndio Sehemu kuu ya Hija.
wasiliana nasiZoezi la Upandaji Miti Miaka 10 Ya Benignis Girls Sec Shool
Misa ya Upadrisho na Ushemasi Kanisa kuu la Mt.Andrea Ifakara
Mhashamu Askofu Salutarisi Libena pamoja na baadhi ya wawakilishi wa watoto 116 waliopata Kipaimara
Mhashamu Askofu Salutaris Libena Kutoka Kulia Akiwa na Mkuu wa Wialaya ya Kilombero wakati wa uwekwaji wa Jiwe la msingi
Adhimisho la Misa ya Shukrani ya Mavuno Dekania ya Mlimba
Mhashamu Askofu Salutaris Libena pichani Pamoja na Pd. Bundala mara baada ya Kupata Daraja Takatifu la Upadri
Jimbo Katoliki Ifakara kwa mara ya kwanza limekutana na kufanya Ibada ya Hija ya Kijimbo na Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Kutukuka kwa Msalaba katika Parokia ya Bikira Maria Bibi yetu wa Kiberege