Adhimisho la Misa ya Shukrani Kumshukuru Mungu kwa Mwaka mmoja tangu Parokia ya Mt.Yohana Mbatizaji V/60 kutangazwa rasmi kuwa parokia. Adhimisho lamisa liliambatana na uwekwaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Jengo jipya la Kanisa.
Jimbo Katoliki Ifakara kwa mara ya kwanza limekutana na kufanya Ibada ya Pamoja Ya hijana Kutukuza Msalaba katika Parokia ya Bikira Maria Bibi yetu wa Kiberege leo tarehe 14/09/2023 ikitanguliwa na Mkesha kwa Sala na Mafundisho mbali mbali kuhusu Maana halisi ya hija na Msalaba. Misa ilitanguliwa na maandamano yaliyoratibiwa na dekani zote za Jimbo.
Kwa furaha kubwa na heshima, Padre Chrispin Tulutulu ameshirikishwa kuwa Padre wa 36 katika Daraja Takatifu la Upadre tangu kuanzishwa kwa Jimbo Katoliki la Ifakara. Habari hii ni kichocheo cha furaha na matumaini kwa waamini wote na jamii kwa ujumla
Katika Misa hiyo, Mgeni rasmi mhashamu Askofu Salutaris Libena alimtakia utume mwema Mwl.Ole ambae anachukuwa nafasi ya mtangulizi wake Mwl.Ndowano