Misa takatifu na tafakari ya pamoja ya watumishi wa Jimbo kwa ajili ya Ujumbe wa KWARESIMA Iliofanyika 21/02/2023 .Ujumbe wa pamoja "TUNAWAOMBEA MJALIWE KUFANYWA IMARA KATIKA UTU ... "
Published date,Ibada pamoja na tafakari ambayo pia ni maandalizi ya kuingia kipindi cha kwaresima. Misa imeongozwa na Mhashamu Baba Askofu Salutaris Libena katika Kanisa la Hija la Huruma ya Mungu Kikwawila-Ifakara a parokia. Kwaresima ni kipindi cha kutafakari zaidi mateso ya Kristo aliye kielelezo cha utu wema. Katika Kwaresima ya mwaka huu tunaalikwa kutafakari sala ya Mtakatifu Paulo anapoiandikia jumuiya ya Waefeso, ambayo ilikuwa changa kiimani. Ni jumuiya iliyohitaji kuwa na elimu ya Mungu na ya Kanisa (rej. Efe 1:15-18; 3:14-19), iliyohitaji umoja hasa kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi (rej. Efe 2:11-22) na iliyohitaji kutiwa nguvu ili kuweza
kushinda kila aina ya udhaifu (rej. Efe 4:17-5:18).
wasiliana nasiZoezi la Upandaji Miti Miaka 10 Ya Benignis Girls Sec Shool
Misa ya Upadrisho na Ushemasi Kanisa kuu la Mt.Andrea Ifakara
Mhashamu Askofu Salutarisi Libena pamoja na baadhi ya wawakilishi wa watoto 116 waliopata Kipaimara
Mhashamu Askofu Salutaris Libena Kutoka Kulia Akiwa na Mkuu wa Wialaya ya Kilombero wakati wa uwekwaji wa Jiwe la msingi
Adhimisho la Misa ya Shukrani ya Mavuno Dekania ya Mlimba
Mhashamu Askofu Salutaris Libena pichani Pamoja na Pd. Bundala mara baada ya Kupata Daraja Takatifu la Upadri
Jimbo Katoliki Ifakara kwa mara ya kwanza limekutana na kufanya Ibada ya Hija ya Kijimbo na Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Kutukuka kwa Msalaba katika Parokia ya Bikira Maria Bibi yetu wa Kiberege